24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Kabendera asomewa mashtaka ya utakatishaji fedha, ukwepaji kodi

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera (39), amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka matatu likiwamo la kutakatisha zaidi ya Sh milioni 173.

Kabendera alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu saa saba mchana na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, Faraja Nchimbi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon walimsomea Mshtakiwa mashtaka matatu ambapo katika shtaka la kwanza kwamba imedaiwa kati ya Januari mwaka 2015 na Julai 2019 maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kabendera na wengine ambao hawapo mahakamani alitoa msaada kwenye genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha.

Katika shtaka la pili mshtakiwa anadaiwa kukwepa kodi, inadaiwa kati ya Januari, 2015 na Julai 2019 maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam bila sababu za msingi alikwepa kulipa kodi Sh 173,247,047.02 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Aidha, katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha, inadaiwa katika tarehe hizo mshtakiwa alitakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zimetokana na zao la kusaidia genge la uhalifu na kukwepa kodi.

Hakimu Rwizile alimfahamisha mshtakiwa kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote. Kesi iliahirishwa hadi Agosti 19 mwaka huu kwa kutajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles