23.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

JUVICUF wamchukulia Pro. Lipumba fomu ya urais

Amina Omari, Tanga

Jumuiya ya vijana ya Chama cha Wananchi (JUVICUF) imemchukulia fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa chama hicho, Pro. Ibrahim Lipumba wakiamini wanaweza kufanya vizuri kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa zoezi hilo ambaye pia ni katibu wa JUVICUF Ilala, Salum Seleman amesema kuwa kutokana na mchakato wa watu waliochukua fomu za kugombea nafasi hiyo ukilinganisha na uwezo wa Profesa Lipumba bado waliona kuna uhitaji mkubwa wa Lipumba kushiriki katika zoezi hilo.

Alisema mfumo wa mchakato ndani ya chama kwa waliochukua fomu ukilinganisha na waliochukua na kurejesha fomu ukilinganisha na uwezo wa Profesa Lipumba wameona bado ana uwezo wa kupeleka mbele maendeleo ya chama hicho lakini pia kuwatumikia Watanzania kwa haki sawa na furaha kwa wote.

“Hata mchuano wa nje kwa nafasi ya urais bado Profesa Lipumba ana sifa nzuri zaidi ya wagombea wa vyama vingine hivyo anahitajhika kuchukua fomu ili kuleta upinzani dhidi ya vyama vingine vya siasa.

“Kitu kilichotusukumu kama vijana kumchukulia fomu Profesa Lipumba ni baada ya kuangalia mchakato wa kuchukua fomu na kurejesha ndani ya chama watu waliochukua na ukimlinganisha na yeye tukaona bado Profesa anahitajika kuchukua fomu kutokana na uwezo mkubwa alionao kuanzia upande wa elimu yake,” alisisitiza Salum.

Mwisho wa kuchukua fomu ya kugombea urais ndani ya chama hicho ni tarehe Julai 24 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,437FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles