25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Jukwaa la Naweza lawapa somo kina mama

Na Mwandishi Wetu- Mwanza

JUKWAA la Naweza limesema iwapo mama ataanza kumpatia vyakula mtoto ambaye hajafikisha miezi sita anaweza kumsababishia magonjwa mbalimbali.

Miongoni mwa magonjwa hayo, ni  pamoja na utapiamlo,kuharibu mfumo mzima wa makuzi yake, ni vema wakazingatia maelekezo nay a wataalamu wa afya.

Jukwaa hilo, limesema atoto wanapougua au kuonyesha dalili za kuumwa, wazazi wanapaswa kuwakimbiza hospitalini,badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji.

Hayo yalisemwa na wataalaamu wakati wa kongamano la afya ya mama na mtoto lilioandaliwa na Mradi wa Usaid Tulonge Afya kwa ajili ya kuwapatia elimu makuzi ya watoto wanawake Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza jana.

Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana alisema kumekuwapo na changamoto ya afya ya makuzi ya watoto kutokana na mila, tabia na desturi za jamii kushindwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu.

“Tumekuwa na tabia kwenye jamii wanafundishana wao kwa wao, wapo wanaoamini mtoto akinyonya maziwa ya mama pekee hashibi, jambo hili sio kweli, anaweza kunyonya maziwa ya mama akashiba bila kula chakula kingine mpaka afikishe miezi sita,” alisema

Alisema wakati mwanamke anapokuwa ananyonyesha mtoto mchanga, anatakiwa asiwe na msongo wa mawazo, ale ashibe ili aweze kuzalisha maziwa ya kutosha.

Mhudumu ngazi ya jamii Kata ya Mhandu, Rachael Mahulu alisema hakuna budi jamii ikaondokana na mila potofu za kuataka kuwalisha watoto wadogo vyakula na dawa kwa misingi ya kuwakuza kumbe kufanya hivyo wanawaharibu.

“Mtoto akiota meno  yanaitwa ya plastikli, wengi wanawakimbiza kwa waganga na kuwapaka dawa za kienyeji, kumfanya hivi ni kosa, nenda hospitali utapewa mwongozo,” alisema.

Ofisa Uwanda kutoka mradi wa USAID Tulonge Afya Wilaya ya Nyamgana, Esuphvat Lewis alisema katika kongamano hilo wamefundisha tabia nne za kiafya katika makuzi ya mtoto ambayo ni pamoja na unyonyeshaji wa maziwa kwa kipindi cha miezi sita.

Zingine ni kuhakikisha mama analala na mtoto kwenye chandarua kimoja angalau mpaka afikishe miezi tisa, mama akiona dalili zozote hatarishi ampeleke mtoto hospitalini na njia za uzazi wa mpango baada ya mtoto kufikisha miezi 24.

Alisema katika mafunzo hayo, wanawake 50 wameshiriki kutoka kata za Wilaya ya Nyamagana.

Baadhi ya wanawake walioshiriki mafunzo hayo, Tatu Ramadhani na Esther Suleiman kwa nyakati tofauti walisema  mafunzo hayo yameweza kuwafungua na kutambua mambo muhimu katika makuzi ya mtoto ambayo walikuwa hawayajui awali..

“Nimejifunza unyonyeshaji wa mtoto na jinsi ya kumlinda na malaria, kiukweli kuna changmoto kubwa wanawake wengi wnashauriana kuwapa watoto uji hasa wa udaga kumbe unaweza kumsbaishia matatizo makubwa,” alisema Tatu mkazi wa Igoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles