29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

JPM: SIJAONA WATU WANAFUNGWA KWA RUSHWA

Na Mwandishi Wetu, Dar

RAIS Dk. John Magufuli, amesema hajaona watu wakifungwa kwa makosa makubwa ya rushwa.

Rais Dk. Magufuli, alitoa kauli hiyo Ikulu, Dar es Salaam jana,baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).

“Rushwa tukiiacha iendelee tutakwama, kwa hiyo nawaomba Watanzania na vyombo vyote vinavyohusika vitoe ushirikiano mkubwa kwa Takukuru, lakini nitoe wito kwenu, sijaona watu wakifungwa kwa makosa ya rushwa.

“Mtu anashikwa na ushahidi, akipelekwa mahakamani ushahidi haupelekwi au unafichwa kwa makusudi au anayeendesha kesi anaamua kutokuusema halafu aliyeshikwa na rushwa anaachiwa… wananchi wanawajua wanaojihusisha na rushwa, ifike mahali watu wanaokutwa na makosa ya rushwa wafungwe,”alisema.

Katika hatu nyingine, Rais Dk. Magufuli aliwaapisha wajumbe wa kamati maalumu ya pili ya wachumi na wanasheria itakayochunguza mchanga wenye madini ulio katika makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini.

Walioapishwa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Nehemiah  Osoro na wajumbe wake ambao ni Profesa Longinus Rutasitara, Dk.Oswald Mashindano, Casmir Kyuki, Andrew Massawe, Gabriel Malata, Usaje Usubisye na Butamo Philip.

Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe hao, Rais Dk. Magufuli alisema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na pia kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998.

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles