25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

JPM: LIGI KUU BARA RUKSA

 WINFRIDA MTOI 

RAIS Dk. John Magufuli (JPM), ametangaza kurejea kwa michezo yote, ikiwamo Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili, kuanzia Juni Mosi, mwaka huu. 

Michezo yote nchini ilisimamishwa na serikali tangu Machi 17, mwaka huu kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya corona. 

Wadau wa soka nchini walikuwa wakisubiri kwa hamu kauli hiyo Rais Magufuli, ikiwa ni baada ya awali kusema anafikiria kuruhusu shughuli za michezo kuendelea kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virus vya corona. 

Akizungumza jana wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, Rais Magufuli, alisema anafahamu kila mmoja anapenda michezo. 

Alisema uamuzi huo unatokana na kuona michezo inasaidia katika kupambana na janga la corona kwa sababu hata katika taaarifa ya waliopata ugonjwa huo, hakuna uhakika kama yupo mwanamichezo aliyefariki. 

“Nafahamu kila mmoja anapenda michezo, hata wabunge wanaenda kwenye michezo, kuna Ligi Daraja la Kwanza, Daraja la Pili, michezo ya Majeshi na mingine, ni lazima watu wafanye michezo. 

“Taratibu za kushangilia na kuangalia zile zinaweza kupangwa na Wizara ya Afya pamoja na Wizara husuka ya michezo ili utaratibu wa nafasi (distance) ukaendelea kuwepo,” alisema Rais Magufuli. 

Baadhi ya viongozi wa klabu za Ligi Kuu Bara, wamepokea kwa mkono miwili tamka hilo la JPM, wakisema wapo tayari kurudi uwanjani kwani walikuwa wakijindaa. 

 “Tupo tayari muda wowote kurudi uwanjani, tunasubiri utaratibu utolewe wachezaji warudi kambini, hapa tunapozungumza mafundi wapo katika uwanja wa mazoezi Chuo cha Sheria wanafanya marekebisho,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli.

Alisema wiki hii walikuwa wanawatembelea wachezaji kuangalia hali zao, wakijiridhisha kila mmoja yupo fiti na sasa wanafanya mipango ya usafiri kwa kocha wao Luc Eymael aliyepo nchini kwao, Ubelgiji.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano wa klabu ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, alisema hawana tatizo lolote, kila kitu kinakwenda vizuri.

“Tumepokea kwa furaha kauli ya Rais, tunafanya utaratibu wa wachezaji wetu waliopo nje ya nchi pamoja na makocha warudi, lakini utaratibu wa kambi ukitolewa, tunaweza kuanza na hawa waliopo Dar es Salaam,” alisema. 

Aidha, Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas, imesema ni ruksa timu kuanza mazoezi.

“Tumepokea kwa unyenyekevu agizo la Rais la ligi na michezo kurejea, huu uamuzi umekuja wakati mwafaka. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tumepokea kwa tabasamu na timu zote za ligi za soka ni ruksa kuanza mazoezi rasmi. Taratibu za kuzingatiwa kiafya zitatolewa,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles