Ariana Grande awakumbuka mashabiki Manchester

0
755

 NEW YORK, MAREKANI 

STAA wa muziki na filamu nchini Marekani, Ariana Grande, ameendelea kuwakumbuka mashabiki zake jijini Manchester waliopata matatizo katika mlipuko wa bomu. 

Tukio hilo la bomu lilitokea siku kama ya leo mwaka 2017 na watu 23 kupoteza maisha huku wengine 139 wakijeruhiwa wakati wa tamasha lake la muziki. 

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26, ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ujumbe wa kusisimua huku akiwakumbuka wale waliopoteza maisha na kujeruhia wakati wa tukio hilo. 

“Nataka kutumia nafasi hii kuwaonesha mashabiki kuwa bado nina upendo wa dhati kwa wale wote ambao waliguswa na tukio hilo, hii ni wiki ambayo nina kumbukumbu kubwa katika maisha yangu, bado ninaumia nikikumbuka, kila siku nimekuwa nikiwaombea na moyo wangu bado upo pamoja nao siku zote,” aliandika mrembo huyo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here