28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

JPM ataka Tanzania iige biashara Vietnam

MTZ DAILY.inddNa Jonas Mushi, Dar es Salaam
RAIS Dk. John Magufuli, amesema Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa Vietnam kwa uzalishaji na ufanyaji wa biashara, ili kuimarisha uchumi.

Rais Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamuhuri Vietinam, Truong Tang Sang, ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, huku akitumia lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza katika ugeni wa kimataifa.
Alisema licha ya Tanzania kuwa na rasilimali za kutosha, bado imebaki nyuma kwenye uzalishaji wa bidhaa na malighafi,  huku Vietnam ambayo ni nchi ndogo kijiografia ikifanya vizuri katika uzalishaji wa mpunga, korosho na samaki.
“Tunatakiwa kuiga mfano wa Vietnam kwa uzalishaji, licha ya kuwa ni nchi ndogo lakini inafanya vizuri kiuchumi.
“Tanzania tuna rasilimali nyingi, mfano tuna mifungo takribani milioni 22, tunashika nafasi ya pili barani Afrika baada Ethiopia, cha kushangaza hatuna viwanda vikubwa vya kuzalisha ngozi wala viatu,”alisema.
Alisema ushirikiano wa nchi hizo, unatakiwa kuwa wa manufaa kwani nchi hiyo ina idadi kubwa ya watu.

Alisema thamani ya biashara miongoni mwa nchi hizo, inafikia Dola za Marekani milioni 300 na lengo ni kufikia dola bilioni moja.
“Vietnam ni ndogo, wana idadi ya watu ipatayo milioni 91.7 hii ni fursa na changamoto kwetu kuhakikisha tunazalisha vyakutosha kuuza kwao,” alisema.
Kwa upande wake, Rais Sang alisema uhusiano uliopo kati ya nchi hizo, ni wa muda mrefu  na unapaswa kudumishwa kwa kuimarisha uhusiano wa kibiashara utakaosaidia maendeleo ya nchi zote mbili.
Amemhakikishia  Rais Magufuli, kuwa Vietnam itaendelea kushirikiana na Tanzania, huku ikitambua mchango mkubwa uliotolewa na watu wa Tanzania walioiunga mkono juhudi za kuiunganisha nchi hiyo na kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti mwaka 1968.

Aliesema kwa kuzingatia mazingira bora ya Tanzania yenye amani na utulivu, Vietnam imedhamiria  Tanzania iwe kituo chake cha kuzifikia nchi nyingine za Afrika Mashariki na sehemu nyingine za Afrika.

Rais Sang, ameomba uhusiano wa nchi hizo, ujielekeze kuongeza biashara, huku akieleza kuwa biashara ya Dola za Marekani takribani milioni 300 haitoshi, na hivyo amependekeza wafanyabiashara wa Tanzania kuunganishwa na wenzao wa Vietnam ili mauzo ya bidhaa kutoka pande zote mbili yaongezeke hadi kufikia Dola za Marekani bilioni  moja ifikapo mwaka 2020.

Alisema nchi yake, iko tayari kutiliana saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano katika biashara, viwanda na kilimo na ametoa mwaliko kwa wakulima wa Tanzania kwenda kujifunza nchini Vietnam.

Rais huyo, alipokelewa katika viwanja vya Ikulu na  kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride maalumu lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pia alipata pia fursa ya kutembelea ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam na kukutana na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Walifanya mazungumzo ya faragha na baadae Kikwete aliwaambia waandishi wa habari Rais Sang ametembelea chama hicho, kutokana na uhusiano wa muda mrefu uliopo baina ya CCM na Chama cha Kikomunisti cha Vietnam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles