JPM amjulia hali Dk. Salim

0
1333
Rais wa Dk. John Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim hospitalini jijini Dar es Salaam jana, alipomtembelea pamoja na mkewe Janeth ili kumjulia hali.

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli jana amemjulia hali Waziri Mkuu mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim anayepatiwa matibabu jijini hapa baada ya kufanyiwa upasuaji.

Pamoja na kutoa pole kwa Dk. Salim, Rais Magufuli akiwa na mkewe Janeth, aliongoza sala ya kumwombea kwa Mwenyezi Mungu waziri mkuu huyo wa zamani ili apone haraka.

Dk. Salim alilazwa hospitalini Januari Mosi, mwaka huu na hali yake inaendelea vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here