23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

JPM akutana na Waziri wa Sweden

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Rais Dk John Magufuli amekutana na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Swedeni, Peter Eriksson na kufanya mazungumzo naye leo Mei 20, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya rushwa na ameeleza dhamira ya Swedeni kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na nchi ya Tanzania.

Aidha katika mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Sweden hapa nchini, Anders Sjoberg, pamoja na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa, Palamagamba Kabudi.

Katika hatua nyingine Rais Dk Magufuli amemuapisha Dk Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada.

Hafla ya kuapishwa kwa Balozi Ulisubisya imefanyika leo Mei 20, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles