27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy Mwalimu: Tunatarajia mashine 60 za kusafishia figo kutoka Saudi Arabia

Ramadhan Hassan

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kupokea mashine 60 za kusafishia figo kutoka Nchini Saudi Arabia ambazo zitafungwa katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi.

Ameyasema hayo Leo Jumanne Mei 21 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (CCM).

Katika swali lake, Mwamoto  amedai kwamba mashine za kusafishia figo zipo sehemu chache  hapa nchini na wagonjwa wanapata shida.

Aidha Mbunge huyo amedai kwamba Serikali haioni kwamba umefika muda wa kila Hospitali ya Rufaa  kuwa na Mashine  ya kusafishia figo.

Akijibu swali hilo Ummy amekiri  kuona ongezeko ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo amedai kwamba Serikali inatarajiwa kupata mashine 60 kutoka Serikali ya Saudi Arabia na kwamba changamoto ambayo itajitokeza ni ukosefu wa wataalamu lakini wameongea na Serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kupeleka wataalamu kwaajili ya kujifunza.

‚ÄúNakubalina nae habari njema tunatarajia kupata zaidi ya mashine 60 kutoka Saudi Arabia changamoto ni upatikanaji wa wataalamu tunaongeza na Saudi Arabia ili tupeleke wataalamu,”amesema

Amesema mashine hizo zitafungwa katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi ambazo wagonjwa wamekuwa wakipata tabu kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles