24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Jordyn Woods azidi kujichongea kwa Kardashian

NEW YORK, MAREKANI

MREMBO Jordyn Woods, anazidi kujiharibiaa kwa familia ya Kardashian baada ya kudaiwa kuwa kwenye uhusiano na aliyekuwa mpenzi wa Khloe Kardashian, James Harden.

Wiki iliopita Khloe alithibitisha kuachana na baba wa mtoto wake ambaye ni nyota wa kikapu katika Ligi ya NBA nchini Marekani, Tristan Thompson kutokana na nyota huyo kutoka na Jordyn Woods.

Harden na Khloe waliwahi kuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miezi nane ambapo ilikuwa mwaka 2015 hadi 2016.

Baada ya Jordyn kuvuruga penzi hilo la Khloe na Tristan, sasa ameamua kuwavuruga tena kwa kutembea na aliyekuwa mpenzi wa Khloe, Harden baada ya kuweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, inasemekana kwamba familia hiyo imemtakia kila la heri Jordyn kwa hicho anachokifanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles