John Witherspoon afariki dunia

0
1150
STAA wa filamu na vichekesho nchini Marekani, John Witherspoon (katikati)

STAA wa filamu na vichekesho nchini Marekani, John Witherspoon, amefariki dunia nyumbani kwake Sherman Oaks huku akiwa na umri wa miaka 77.

Chanzo cha kifo chake hadi sasa hakijawekwa wazi, lakini familia uliuambia mtandao wa Deadline kuwa, amepoteza maisha huku akiwa kwenye kitanda chake.

“Ni taarifa mbaya kwamba ndugu yetu mpendwa, baba wa familia, John Witherspoon, mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanajituma sana kwenye biashara zao amefariki dunia leo (jana).

“Wote tumebaki midomo wazi, hivyo tunawaomba mashabiki wote watumie hata dakika moja kwa ajili ya kumuombea na kisha baada ya hapo tutakuwa tunayafurahia maisha yake kwa pamoja,” ilisema familia hiyo.

Msanii huyo aliwahi kufanya filamu mbalimbali kama vile The Jazz Singer ya mwaka 1980, zingine ni Vampire In Brooklyn, Hollywood Shuffle, Boomerang, I’m Gonna Get Your Sucka, Soul Plane, The Meteor Man na zingine nyingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here