Watoto wamchanganya Rihanna

0
1055

NEW YORK, MAREKANI 

STAA wa muziki wa pop nchini Marekani, Rihanna Fenty, ameonesha dalili ya kuhitaji mtoto baada ya rafiki yake Jennifer Rosales kujifungua mtoto wa kiume na kisha kumposti kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 31, alianza kwa kumpongeza rafiki yake huyo kwa kujifungua salama na kisha kusema, anatamani siku moja na yeye aje kuitwa mama.

“Nina furaha kuona rafiki yangu amefanikiwa kupata mtoto, mimi nitakuwa shangazi yake, hivyo lazima ajue kuwa ninampenda sana.

“Ninakuwa na furaha nikiwa nawaona watoto wadogo, ninaamini na mimi ipo siku nitakuja kuitwa mama, sijui ni lini lakini muda utafika,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here