JOHN CENA ATENGANA NA NIKKI

0
967

LOS ANGELES, MAREKANI


BINGWA wa mchezo wa mieleka wa WWE, John Cena, ametangaza kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Nikki Bella, baada ya miaka sita ya uchumba wao.

Wawili hao walikuwa pamoja tangu mwaka 2012 huku wakifanya mambo mbalimbali yaliyowatambulisha kama ‘Total Diva na Total Bellas’.

Baada ya kufikia tamati wawili hao jana walitangaza rasmi kuwa wameachana. “Baada ya kufanya mambo mengi katika miaka sita tuliyoishi, Nikki Bella na John Cena, tumeamua kutengana.”

Nyota hao walitoa taarifa hiyo wakidai kuwa licha ya kufanya uamuzi huo mgumu, bado wataendelea kufanya kazi pamoja kwa kuheshimiana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here