22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

WEMA AMTAMANI MTOTO WA HAPPINESS MAGESE

NA SHARIFA MMASI


MWIGIZAJI mahiri nchini, Wema Sepetu, ameweka hisia zake za kutamani kuishi na Kairo, ambaye ni mtoto wa Happiness Magese, aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2001.

Wema alionyesha hisia hizo kupitia moja ya ukurasa wa kijamii wa Magese, baada ya dakika chache kutupia picha ya mtoto wake.

“Da Happy ukija si utanigaia huyu apa hata siku tatu, naomba tafadhali, ila sijui maana huyu ni zaidi ya roho kwako, aaah mimi nitakuja kukaa na wewe tu hata wiki ili nimng’ate ng’ate mashavu,” aliandika Wema.

Baada ya ujumbe huo, Magese aliibuka na kumjibu Wema kwa kumsihi asikate tamaa badala yake awe na subira kwani siku moja Mungu atamfanyia maajabu na yeye aitwe mama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles