23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YASHIKILIA PASPOTI YA DIAMOND

 

JESSCA NANGAWE Na RAMADHAN HASSAN- DODOMA


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewatia mbaroni na kuwahoji wasanii watatu wa Bongo Fleva, akiwamo nyota wa kimataifa, Naseeb Abdul, maarufu Diamond Platinumz.

Wengine ni Faustine Charles (Nandy), William Lyimo (Billnas) na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Hatua ya kukamatwa kwa wasanii hao imekuja baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii video za faragha kinyume cha maadili.

Wasanii hao walihojiwa kwa saa kadhaa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Nandy na Bilinass walihojiwa kutokana na video yao ya faragha huku Diamond naye akihojiwa kwa kusambaza video yake akiwa faragha na mama wa mtoto wake, Hamisa Mobetto.

Baada ya wasanii hao kukamatwa juzi, walitakiwa kwenda tena kuripoti jana na waliachiwa baada ya kudhaminiwa wakitakiwa kuripoti Aprili 20, mwaka huu huku hati za kusafiria na simu zao zikishikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, aliambia MTANZANIA kuwa Diamond alishikiliwa na polisi kwa mahojiano kutokana na picha zisizo na maadili.

Mbali na msanii huyo, pia alisema mwingine aliyekamatwa kwa mahojiano ni mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto na wasanii Nandy na Billnas.

Alisema baada ya Diamond kuhojiwa, alipewa dhamana jana huku uchunguzi zaidi ukiwa unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi.

“Alihojiwa na akapewa dhamana, upelelezi unaendelea,” alisema Mambosasa.

Jana katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema polisi inawashikilia Diamond na Nandy ambao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kusambaza picha zisizo na maadili kwenye mtandao.

Wasanii hao wanadaiwa kusambaza picha hizo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

Waziri Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM), aliyehoji jinsi gani Serikali imejipanga kupambana na wasanii wa muziki na vikundi vya watu wanaosambaza lugha za matusi mitandaoni.

“Kwenye mitandao kuna uhamasishaji wa ushoga, usagaji, kutukana matusi mithili ya bomu la nyuklia sio maadili na desturi ya Mtanzania.

“Lakini vitendo hivi vimekithiri kwenye mitandao ya kijamii, wapo mashoga maarufu wanajitangaza kwenye mitandao ya kijamii, mfano kuna mtu anaitwa James Delicious.

“Kuna vikundi vya matusi kwenye mitandao ya kijamii kwa mfano Team Wema, Zari, Daimond, Shilole, hawa wamekuwa wakitukana matusi mno kwenye mitandao ya kijamii,” alieleza Mlinga.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles