29.7 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Polisi, DCPC waunda Kamati kusimamia usalama wa Waandishi wa Habari

Na Sabina Wandiba, Mtanzania Digital

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) wameunda Kamati ndogo itakayosimamia na kufuatilia ulinzi na usalama wa Waandishi wa Habari wanapokuwa kazini.

Kamati hiyo yenye wajumbe sita imeundwa Machi 22, 2024 kwenye mdahalo wa majumuisho kati ya DCPC na Jeshi la Polisi.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Malulu, ambaye pia ni RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Askofu Emaus Mwamakula na Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu.

Wengine ni Wakili Mkumbo Emmanuel, Katibu Mkuu wa DCPC, Fatma Jalala na Bakari Kimwanga (Mwanachama wa DCPC).

Kuundwa kwa Kamati hiyo ni matokeo ya midahalo mitatu kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa Waandishi wa Habari, lakini pia pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria.

Katika mdahalo huo Kamanda Muliro ameahidi kuwa polisi, itaendelea kusimamia haki kama vile zinavyotambuliwa Kitaifa na Kimataifa na kwamba anawahakikishia waandishi wa habari kuwa salama.

Midahalo hiyo iliyoanza Novemba 2023 na kumalizika Februari 2024, kuratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) chini ya udhaminiwa na Shirika la IMS, ilihusisha Kanda Maalum (Ilala ikiwemo), Temeke na Kinondoni, ambapo maazimio kadhaa ya kiutendaji yalifikiwa.

Miongoni kwa maazimio hayo ni kuwepo kwa mabonanza ya kimichezo kwa lengo la kujenga ukaribu na kuhakikisha usalama wa Waandishi wanapokuwa kazini na hata katika operesheni mbali mbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles