28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Jenerali Mabeyo awaonya wanaotoa kauli za uchochezi

Maregesi Paul

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, amesema hivi sasa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linafuatilia kwa karibu kauli za uchochochezi zinazotolewa na baadhi ya watu nchini.

Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo mjini hapa leo Jumamosi Aprili 13, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mji wa Serikali katika eneo la Mtumba mjini Dodoma mbele ya Rais Dk. John Magufuli.

Ingawa hakutaja kauli hizo za uchochezi zinatolewa na akina nani, Jenerali Mabeyo alisema JWTZ liko tayari kukabiliana na tishio lolote la amani nchini.

“Pamoja na hayo, hali ya usalama wa nchi iko tulivu kwa kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi jirani na uwepo wa migogoro katika nchi zinazopakana na Tanzania, JWTZ tuko tayari kukabiliana na tishio lolote la amani litakalosababishwa na migogoro katika nchi jirani,” amesema.wl

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binirith Mahenge aliwakaribisha wananchi wakawekeze mkoani Dodoma kwa kuwa kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles