27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Kim Kardashian kurudi shule, warembo Bongo wanakwama wapi?

SWAGGAZ RIPOTA

HAKUNA ambaye alikuwa anajua kuwa mrembo tajiri duniani Kim Kardashian, amerudi shule labla watu wake wa karibu pekee mpaka wiki hii alipoivunja habari hiyo katika jarida la Vogue.

Kim Kardashian, ameweka wazi kuwa tayari ameingia darasani kusomea sheria katika ngazi ya shahada akitarajia kuhitimu mwaka 2022 chini ya uangalizi na usimamizi wa kampuni ya mawakili ya San Francisco California nchini Marekani.

Mrembo huyo amekuwa gumzo mtandaoni kwani hakuna aliyedhani mtu mwenye hadhi kama yake kukumbuka kurudi shule jambo ambalo mashabiki na mastaa wenzake wamempongeza.

HANA CHA KUPOTEZA

Pongezi nyingi zilizotolewa na mashabiki, zimeonyesha wazi kuwa mwanamitindo huyu hana cha kupoteza endapo angeamua kuacha kusoma. Ana kila kitu ambacho mrembo kama yeye anahitaji kuwa nacho.

Kwanza ni mrembo ambaye amekuwa na mvuto mbele ya macho ya wanamume wengi wanaomtazama kwa jicho la mahaba hali kadharika Kim Kardashian ni ‘role model’ wa warembo wengi wanaochipukia kwenye tasnia ya mitindo akiwamo staa wa filamu hapa Wema Sepetu.

Pili Kim ni tajiri, utajiri alioupata kutokana ujasiliamali wake katika bidhaa za urembo zinazofanya vizuri sokoni hivyo hana shida ya fedha kiasi cha kuhitaji kurudi shule ili apate ajira kwenye sekta ya sheria.

Mwanamitindo huyu pia ni mama wa watoto watatu, Saint, North, Chicago aliozaa na mumewe rapa Kanye West ambaye wiki chache zilizopita alimkataza kutumia ukurasa wa Instagram kwa matangazo ya biashara na akampa shilingi bilioni 2 kama fidia.

Kwa hiyo unaweza kuona kuwa kwake shule ilikuwa siyo kitu cha lazima ila imembidi kusoma kwa sababu anahitaji kuongeza uelewa wa mambo mbalimbali ya kisheria ambayo yanaweza kumsaidia yeye na watu wengine.

KWANINI ASOMEE SHERIA

Kwa muda mrefu Kim, amekuwa akisaidia baadhi ya watu ambao wana changamoto za kisheria huku kwenye mahojiano na jarida la Vogue, ameendelea kukazania lengo lake litimie.

Mwanamitindo huyo, amekuwa mstari wa mbele katika kujihusisha na mambo ya kisheria hasa kuhusu kubadili sheria na hukumu za magereza nchini Marekani ambazo amekuwa akidai zina mapungufu.

WAREMBO BONGO WANAKWAMA WAPI?

Miongoni mwa ishu zinazowakwamisha mastaa wengi wakike Bongo ni kuwa na elimu ndogo kiasi cha kushindwa kuhimili umaarufu na fedha wanazopata, mwisho wa siku wanaishia kuibiwa wajanja.

Warembo wengi wanaridhika na umaarufu na kusahau kujiendeleza kielimu ili kuongeza uelewa na mambo mbalimbali ya sanaa zao ili waweze kujisaidia na kuwasaidia wengine wenye uhitaji.

Hili la Kim, linaweza kuwapa nguvu warembo wetu Bongo kuacha kubweteka na ustaa walionao bila kuwa na uelewa wa mambo ya biashara ya sanaa kwa kuongeza elimu zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles