JANET JACKSON AWEKA REKODI YA MTU MASHUHURI ALIYEJIFUNGUA MTOTO AKIWA NA UMRI MKUBWA

0
833
janet-jackson
Janet Jackson akiwa na mumewe Wissam Al Mana

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani , Janet Jackson ameweka rekodi ya kuwa mtu mashuhuri aliyejifungua mtoto akiwa na umri mkubwa baada ya kujifungua  mtoto wa kiume akiwa na miaka 50.

Kwa taarifa zilizopo, mwanamuziki huyo na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto huyo waliyempa jina la Eissa Al Mana.

Janet ambaye alizaliwa Mei 16, 1966 huko Gary, Indiana na dada wa aliyekuwa mfalme wa Pop Michael Jackson, alijifungua salama bila tatizo lolote na kwamba yeye na mwanaye wanaendelea vizuri.

Mwanadada huyo aliyefunga ndoa mwaka 2012 amezipita rekodi za watu wengine mashuhuri waliowahi kupata watoto wakiwa na umri mkubwa kama vile mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry ambaye alijaliwa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47 miaka mitatu iliyopita.

Pia rekodi ya mke wa John Travolta, Kelly Preston, aliyejifungua mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.

Lakini yote hii hamfanyi Janet kuwa mwanamke wa kwanza duniani kuzaa mtoto akiwa na umri mkubwa kwani yupo Daljinder Kaur kutoka India aliyepata mtoto akiwa na umri wa miaka 70.

INDIA-HEALTH-FERTILITY-IVF
Daljinder Kaur (70) akiwa na mumewe Mohinder Singh (79) wakiwa na mtoto wao Arman

Katika kazi za uimbaji, Janet alizindua albamu yake ya kwanza 1982, ana albamu 11, ameshinda tuzo za Grammy mara saba, na amekwisha olewa mara tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here