32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii yaaswa kununua bidhaa mtandaoni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JAMII imetakiwa kuendelea kuwa na imani na wafanyabiashara wanaouza bidhaa kupitia mitandao kwa kuwa ni moja ya njia rahisi ya kuwafikia wateja waliokuwa katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika warsha ya wauzaji wa magari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Meneja wa Masoko wa Mtandao wa Cheki kuwakutanisha wafanyabiashara wa magari Tanzania, Mori Bencus, alisema wananchi wana tatizo kubwa la kutowaamini wafanyabiashara wa mitandao na wengine wakidhani kuwa ni matapeli jambo ambalo si kweli.
“Awali lilikuwapo tatizo la uaminifu mtu anaona kama matangazo ya mitandaoni ni utapeli tu ila sasa kidogo imani imeongezeka kwa wateja wa mitandao jambo ambalo limechangiwa na wauzaji kuwa waaminifu. Hii inatusaidia kuongeza wateja katika maeneo mbalimbali,” alisema Bencus.
Alisema kupitia warsha hiyo wafanyabiashara watapewa elimu na jinsi ya kutumia njia sahihi ya kumfikia mteja kwa wakati na kuwakumbusha kuuza magari yasiyokuwa na hitilafu za ufundi.
Alisema mtandao wa Cheki.co.tz ulianzishwa Septemba mwaka jana na hadi sasa umewaunganisha watu 15,000 kwa wafanyabiashara 67 wa magari waliosajiliwa Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema zaidi watu 30,000 mpaka 60,000 wanatembelea mtandao huo kwa mwezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles