28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

JAJI KIONGOZI AWANYOSHEA KIDOLE MAJAJI, MAHAKIMU

Na Magreth Kinabo-Mahakama ya Tanzania 


                 

JAJI Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Ferdinand Wambali, amewataka Majaji na Mahakimu kuzingatia maadili ya uhakimu na utumishi wa umma.

Alisema hawana budi  kutenda haki kwa wakati  wanapokuwa kwenye majukumu yao.

Wambali  amewataka majaji, mahakimu kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni za utendaji na za utumishi wa umma kama njia ya  kukidhi mahitaji ya wananchi wanaowahudumia.

Alitoa kauli hiyo  Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alipozungumza na baadhi ya majaji na  mahakimu katika   ofisi ndogo za Bunge.

“Suala la maadili lilianza tangu enzi za kale, jamii ilikuwa inajiwekea maadili, kuwapo   maadili ni heshima na utii, tabia ya uaminifu, uwajibikaji na kufuata  utaratibu kila unapotekeleza kazi,” alisema Jaji Wambali.

 Alisema suala la maadili ni muhimu katika kupambana na rushwa kwa sababu  linafanya jaji na hakimu awe na tabia njema mbele ya jamii.

Alisisitiza kuwa  kazi hizo zinahitaji uadilifu na mtu mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu.

Naye  Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Beatrice Mutungi  alisema lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili changamoto za kada hizo na kubadilishana uzoefu wakati wa kutatua changamoto hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles