IRAN YAONYA ITAREJESHA MIPANGO YAKE YA NYUKILIA

0
1017

TEHRAN, IRAN


WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameonya nchi yake haitasita kurejesha mpango wake tata wa silaha za nyukilia.

Amesema Iran itarejesha mpango huo haraka iwezekanavyo iwapo Marekani itajiondoa kutoka makubaliano ya kihistoria ya nyuklia yaliyofikiwa mwaka 2015.

Rais Donald Trump wa Marekani amepanga Mei 12 kuwa siku ya mwisho kwa mataifa ya Ulaya kufikia makubaliano yanayoitaka Iran kusitisha mipango yake ya nyukilia, hatua ambayo inaenda sambamba na kulegezwa vikwazo dhidi ya nchi hiyo.

Trump amekuwa akipinga makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 wakati wa mtangulizi wake Rais Barack Obama, akisema hayaibani Iran kuachana na mpango huo, kauli ambayo imekuwa ikiungwa mkono na Israel

Kauli ya sasa ya Zarif inasisitiza onyo lililotolewa mwezi uliopita na Rais wa Iran Hassan Rouhani

Rais huyo mwanamageuzi aliapa kuwa Marekani itajuta iwapo itajiondoa kwenye makubaliano hayo na kuwa Iran itajibu vikali hatua hiyo ndani ya wiki moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here