27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Iran yaonya hatari ya kutokea ‘vita vya ukanda’

 TEHRAN, IRAN

IRAN imeonya kuwa mapigano mapya kati ya majirani zake Azerbaijan na Armenia yanaweza kuongezeka na kuwa vita pana ya ukanda.

Rais Hassan Rouhani alisema ana matumaini “ya kurejesha utulivu” katika eneo hilo kufuatia siku kadhaa za mapigano makali yanayosababishwa na eneo lenye mgogoro la Nagorno-Karabakh.

Eneo hili ni sehemu rasmi ya Azerbaijan lakini inadhibitiwa na jamii ya Waarmenia.

Mapigano ya sasa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa, na pande zote mbili zimelaumiana kwa machafuko .

“Lazima tuwe waangalifu kwamba vita kati ya Armenia na Azerbaijan isiwe vita vya kieneo. Amani ndio msingi wa kazi yetu na tunatarajia kurejesha utulivu katika eneo hili kwa njia ya amani,” Rais Rouhani alisema Jumatano.

Rais Rouhani pia alisema “haikubaliki kabisa” kwa makombora yoyote yaliyokosea njia kutua kwenye ardhi ya Irani.

Maoni yake yalifuatia ripoti kwamba makombora yalikuwa yametua kwenye vijiji vya Irani, karibu tu na mpaka wake wa kaskazini na Armenia na Azerbaijan.

“Kipaumbele chetu ni usalama wa miji na vijiji vyetu,” Rais Rouhani alisema.

Kamanda wa Walinzi wa Mipaka wa Irani, Qasem Rezaei pia alisema vikosi vyake vimejitatiti.

“Tangu kuanza kwa mzozo … makombora kadhaa ya roketi na roketi zimegonga eneo la [Iran],” alisema, kulingana na shirika la habari la Tasnim.

“Walinzi wetu wa mipaka wako macho na wamehamia kwenye maeneo muhimu. Wanafuatilia kikamilifu na kudhibiti mipaka.”

Siku ya Jumatano, Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitoa wito wa kumaliza mapigano, ambayo alielezea kama “janga”.

“Tuna wasiwasi sana. Tuna matumaini kuwa mzozo huu utamalizika katika siku za hivi karibuni. Watu wanakufa na kuna hasara kubwa pande zote mbili,” alisema kwenye mahojiano kupitia televisheni.

Putin pia alifanya mazugumzo mafupi ya simu na rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev Jumatano, Kremlin ilisema.

Urusi ni sehemu ya muungano wa kijeshi na Armenia na ina kituo cha jeshi nchini humo. Hatahivyo, pia ina uhusiano wa karibu na serikali ya Azerbaijan.

Marekani, Ufaransa na Urusi kwa pamoja wamelaani mapigano huko Nagorno-Karabakh na wametaka mazungumzo ya amani, lakini mzozo huo hauoneshi dalili zozote za kupungua.

Siku ya Jumatano Azerbaijan ilisema Waziri wa Mambo ya nje Jeyhun Bayramov atakutana na wapatanishi wa kimataifa huko Geneva siku ya Alhamisi.

Armenia ilijibu kuwa “haiwezekani kufanya mazungumzo kwa mkono mmoja na kuendelea na shughuli za kijeshi kwa mkono mwingine”, na kwamba waziri wake wa mambo ya nje hatakutana na Bwana Bayramov huko Geneva.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles