Iran, Israel zaparurana UNGA

0
826

NEW YORK, MAREKANI

Mataifa  ya Israel na Iran yamelumbana vikali katika hotuba zao kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), unaoendelea mjini New York, nchini Marekani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran (IRNA), Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mohammad Javad Zarif, amelaani madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema ni madai ya uchafu.

Waziri Zarif amesema Netanyahu ni mtu muongo ambaye hawezi kuacha kusema uongo. Matamshi ya Waziri Zarif yamekuja baada ya juzi Waziri mkuu huyo wa Israel akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alidai kwamba, Iran ina ghala la siri la silaha za atomiki nje ya mji wao mkuu wa Tehran, ambapo pia aliwataka waangalizi wa umoja huo kufanya uchunguzi.

Bado haijafahamika ikiwa tangazo hilo la Netanyahu limetoa mwanga mpya kuhusu kile ambacho tayari wanakifahamu waangalizi wa Umoja wa Mataifa au kimethibitisha kwamba Iran inakiuka makubaliano ya nyukilia ya mwaka 2015 yaliyofikiwa kati ya nchi hiyo na nchi zenye nguvu.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Waziri Zarif amesema Israel ndio nchi pekee ambayo haijatangaza mpango wake wa silaha za nyuklia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here