27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

IFM tawi la Simiyu kuanza Machi mwakani

Derick Milton, Simiyu

Uongozi wa Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) umesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2020 tawi lake la Simiyu litaanza rasmi kufanya kazi kwa kupokea wanafunzi wenye kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Astashahada (cheti) na shahada (Diploma).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Thadeo Sata, mbele ya Naibu Waziri wa Fedha Dk. Ashatu Kijaji katika ziara yake ya siku moja kukagua ujenzi wa tawi hilo katika kijiji cha Sapiwi Wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu.

Profesa Sata amesema ujenzi wa majengo mbalimbali kwenye tawi hilo unaendelea chini ya Mkandarasi Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Kagera kwa gharama ya Sh bilioni tatu.

“Ujenzi wa majengo kwenye tawi hilo ulianza julai mwaka huu na kwa awamu ya kwanza ambao inagharimu Sh milioni 900, jengo la utawala limefikia asilimia 62 na madarasa asilimia 92,” amesema Profesa Sata.

Amesema udahili wanafunzi utaanza Machi mwakani ambapo wataanza na wanafunzi 1,000 kwa masomo ya ngazi hizo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Kijaji, amemtaka Profesa Sata, kutumia vizuri nafasi aliyonayo kuhakikisha bweni linajengwa na chuo kinaanza kazi Machi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles