23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

IDADI VIFO VYA MAFURIKO DAR YAONGEZEKA

KOKU DAVID na FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kiluvya, Teddy Narasco (8), amefariki dunia baada ya kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Jumatano na Alhamisi wiki hii.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kifo hicho kilitokea maeneo ya Kiluvya kwa Komba, wakati mwanafunzi huyo akijaribu kujiokoa kutokana na maji mengi yaliyokuwa yamezingira katika nyumba yao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Kifo cha mwanafunzi huyo ni cha tatu, baada ya juzi Jeshi hilo kutangaza kifo cha mtu mmoja aliyefariki saa 12 jioni kutokana na mvua hizo katika maeneo ya Mwananyamala Kisiwani, baada ya kupokea taarifa ya kifo cha mwanamume mmoja ambaye hakufahamika jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 au 35, aliyesombwa na maji ya Mto Ng’ombe, uliofurika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kifo kingine kilitokea saa 12 jioni maeneo ya Tabata Kimanga, baada ya mwili wa mtu jinsia ya kiume kuonekana unaelea katika maji ndani ya Mto Tenge na Jeshi hilo lilisema askari walifuatilia na kugundua kuwa kimetokana na mvua hizo.

Jeshi hilo lilisema mwili huo haukutambulika jina lake wala unapotokea na unakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 au 22, umehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

DAR ES SALAAM

Katika hatua nyingine, Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) wamefanya ukaguzi katika Daraja la Mbezi Kibanda cha Mkaa lililomeguka kutokana na mvua hizo zilizosababisha pia uharibifu wa miundombinu ya barabara, nyumba na hali ya usafiri kuwa mgumu.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, alisema katika wilaya yake hakuna athari kubwa zilizotokana na mvua hizo na baadhi  ya wakazi waliathirika baada ya nyumba zao kujaa maji, huku nyingine zikibomoka.

Pia alisema hakuna taarifa za vifo vilivyotokana na mvua hizo, isipokuwa baadhi ya vivuko katika maeneo ya Mabibo na Goba vilikatika kutokana na kasi ya maji.

“Katika wilaya yangu hatukupata madhara makubwa, labda katika Daraja la Mbezi Kibanda cha Mkaa, daraja hilo limemeguka kidogo, lakini Tanroads wameshafika na kuliangalia ili kuona kama linaweza kusababisha madhara au la na kwamba wao wenyewe kama wataalamu watajua cha kufanya,” alisema.

Makori alisema katika maeneo ya Mburahati na Tandale kuelekea Sinza Kijiweni pia kulijaa maji na baada ya mvua kupungua barabara ziliendelea kutumika kama kawaida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles