24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ibaada ya kumuenzi Hayati Sokoine kufanyika Aprili 12

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

IBAADA maalum ya kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati Edward Sokoine inatarajiwa kufanyika Ijumaa Aprili 12,mwaka huu ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki.

Hayati Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika vipindi viwili wakati wa uongozi wa Awamu ya Kwanza ambapo alizaliwa Agosti 01, 1934, kijijini Enguik, Monduli Juu wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Alifariki Aprili 12, mwaka 1984 katika eneo la Dakawa mkoani Morogoro akitokea Bungeni jijini Dodoma ambapo enzi za uhai wake pia amewahi kuwa Mbunge wa Monduli, Naibu Waziri na Waziri katika Wizara mbalimbali katika Serikali ya awamu ya kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi Machi 28, jijini Dodoma, Msemaji wa Familia ya Hayati Sokoine, Lembris Kipuyo amesema ibada hiyo itafanyika katika Kijiji cha Enguik Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha.

“Nawaalika Watanzania wote kwenye ibada maalum iliyoandaliwa na famia kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakayofanyika Ijumaa Aprili 12, 2024 saa 3 Asubuhi, katika Kijiji cha Enguik, Monduli Juu mkoani Arusha,” amesela Kipuyo.

Amesema ibada hiyo ya kumbukumbu ya Hayati Sokoine itawashirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa Taasisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine, ni kuenzi mema aliyoyafanya, kwani aliacha alama kubwa ambayo Taifa linamkumbuka hadi leo.

“Taasisi hiyo imejikita katika masuala ya elimu, kilimo, uhifadhi wa mazingira, vyanzo vya maji pamoja na afya,” amesema.

Amesema hayati Sokoine alikuwa mzalendo wa kweli, alipenda Taifa lake na wananchi wake, alihakikisha kwamba rasilimali za nchi zinatumika na Watanzania wote, aliwatumikia wananchi bila kubagua na alikuwa na hofu ya Mungu katika kufanya kazi zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles