25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

HOTELI YA BLUE PEARL YAFUNGWA, YADAIWA KODI BIL 5.7

Mfanyakazi wa Kampuni ya Udalali ya Yono akifuta maandishi ya hoteli ya Blue pearl baada ya kufungwa kutokana na kudaiwa kodi.

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Udalali ya Yono, imeifunga Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Novemba 9, kutokana na kudaiwa kodi ya pango ya Sh bilioni 5.7.

Hoteli hiyo inadaiwa kodi hiyo na Kampuni ya Ubungo Plaza ambayo inamilikiwa kwa ubia na Shirika la Bima la Taifa (NIC), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni wa PSPF.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scholastika Kevela, amesema walipewa kazi ya kuifunga hoteli hiyo na hatua nyingine za kisheria zitafuata endapo watashindwa kulipa deni hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ubungo Plaza, Harun Mgude, amesema mpangaji huyo alikuwa na mkataba wa miaka 15 tangu mwaka 2006 lakini tangu mwaka 2014 hajalipa kodi ya pango.

Katika kuonyesha hawatanii, Kampuni ya Yono walifuta maandishi katika mabango ya hoteli hiyo huku baadhi ya ya wageni waliokuwa wamelala hotelini hapo wakiwa na na taharuki wasijue cha kufanya wakati wengine wakijiandaa kuondoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles