25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Hospitali ya KCMC kuanza upandikizaji mbegu

Aveline Kitomary- Kilimanjaro

HOSPIATALI ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini(KCMC), kwa mara ya kwanza nchini inataraji kuanza kutoa huduma za upandikizaji mbegu kwa watu ambao mirija yao inafanya kazi vizuri lakini  wameshindwa kupata ujauzito.

Akizungumza mkoani Kilimanjaro wakati wa kampeni za ‘tumeboresha Sekta ya Afya’ iliyoandaliwa na maofisa habari wa taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Benjamin Shayo alisema uhitaji wa huduma hiyo ni mkubwa.

“Tulianza kutoa huduma za ushauri na matibabu ya kawaida tangu mwishoni mwa mwaka 2018 na kwa wiki tunafanya kliniki mara moja siku Alhamisi, tulianza kama huduma za kutoka na kuingia, tulianza na watu kama watano na kutokana na wingi wa watu na maongezi kuchukua muda mrefu tulianza na watu wanne mpaka watano lakini kutokana na uhitaji kuwa mkubwa kwa sasa tunaona watu 10 hadi 15 kwa siku.

“Mpaka sasa uwezo tulionao ni wa vipimo vya  kugundua kama unatatizo kwenye homoni, kuangalia mirija na matibabu ya kutoa  dawa za kumeza, mwaka huu tunaanza kupandikiza mbegu kwa wale ambao mirija inafanya kazi vizuri lakini bado wanashindwa kupata ujauzito baada ya hapo mpango ni kupandikiza mimba,”alisema Dk Sh ayo.

Alisema matatizo ya uzazi kwa kiasi kikubwa yanatokana na vichoche vya homoni na mirija kuziba.

“Hapa tunapata watu wa kuanzia miaka 30 mpaka 45, kitaifa wanasema tatizo hili ni asilimia 8 hadi 15. Tatizo la ugumba halina sababu ya moja kwa moja ila baadhi ya visababishi ni mirija ya kupitisha mayai kuziba, shida yakutunga mimba kwenye kizazi kuna za maumbile kama uke kubana,”alisema.

Aliwasahuri watu kuacha matumizi ya vilevi kwasababu vinaharibu ubora wa mbegu za kiume na za kike.

Akizungumza mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali, Dk Sarah Urasa, alisema wamefanikiwa kujenga na kufungua kinu cha kufua hewa ya oksijeni na nitrogen ambayo inauwezo wa kuzalisha mitungi 400.

“Hii ni hospitali ya kwanza kuwa na aina hii ya kinu, hewa ya oksijeni inasaidia wagonjwa ambao wanatatizo la kupumua na pia wale wanaofanyiwa upasuaji kwa kutumia dawa ya usingizi

“Nitrogen inakazi ya kuhifadhi sampuli zinazochukuliwa kwa wagonjwa, kutoa tiba ya ngozi, kukata vioteo vilivyoko kwenye ngozi au magonjwa mengine ya sehemu za uzazi pia inatumika kuhifadhia mbegu za kike na za kiume kwa watu wenye matatizo ya uzazi na inatumika na wenzetu wanaohusika na afya ya wanyama,”alieleza Dr Urasa.

Alisema mafanikio mengine ni kuendelea kuzalisha maji tiba (dripu) kwaajili ya hospitali hiyo na hospitali zingine. 

“Mafanikio mengine ni kuzalisha mafuta maalum kwaajili ya watu wenye matatizo ya ngozi kwa kujikinga na mionzi hatarishi ya jua, tuliingia makubaliano na MSD ya kusambaza mafuta kwa maeneo yote yenye uhitaji hata hivyo kwasasa tunasambaza wenyewe na tumefanikiwa kufikia mikoa 25 lakini  MSD itachukua jukumu la kusambaza,”alisema.

Kwa mujibu wa Dk Urasa hospitali hiyo inatarajia kuanzisha kitengo ambacho kitakuwa kinatoa huduma ya matibabu ya moyo.

“Idadi ya wagonjwa hospitalini hapa  ni 1,000 kila siku hivyo wagonjwa ni wengi mwaka jana tulianza kutumia mfumo rasmi wa utunzaji kumbukumbu ili kurahisisha huduma

“Katika Kliniki ya moyo kuna wagonjwa 60 na wengine wanakuja kwenye kliniki ya ndani bila kwenda kwenye kliniki ya moyo na kwa kila mwezi tunawapa rufaa wagonjwa 15 hadi 20 kwenda Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hao wenye matatizo ya moyo wanaohitaji upasuaji ila wanaotibiwa na dawa wako hapa tunaona wanahitaji kitengo chao.

“Watoto wanaozaliwa na matatizo ya moyo pia wanapelekwa Dar es salaam ni  kama watano kwa mwezi wachache wanapata matatizo ya mfumo wa  hewa

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles