24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

HOSPITALI TANO ZA RUFAA KUJENGWA -MAJALIWA

NA AZIZA  MASOUD,Dar es Salaam.


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali inatarajia kuanza kutekeleza miradi mikubwa mitatu ikiwamo ujenzi wa hospitali za rufaa tano zitakazojengwa katika kanda kwa msaada  wa   Korea ya Kusini.

Alitoa kauli hiyo Ikulu, Dar es Salaam jana baada ya mazungumzo  na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Lee Nak-Yon ambaye yupo nchini kwa ziara ya  kazi ya siku tatu.

Majaliwa  alisema miongoni mwa mambo  aliyozungumza na kiongozi huyo ni   namna bora ya kuendeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo ambako walikubaliana kuanza kutekeleza ujenzi wa miradi mitatu mikubwa.

“Mbali na miradi hii iliyopo sasa  tunatarajia kutekeleza miradi mingine mitatu  ikiwamo ya msisitizo wa kuimarisha   sekta ya afya kwa kujenga hospitali nyingine tano za rufaa kwenye kanda zote,nayo ni maeneo ambayo tumeyazungumza leo(jana),”alisema Majaliwa.

Alisema miradi mingine  ni ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi  Mwanza, lenye urefu wa mita 3,200  na kuimarisha mradi wa barabara ya Chaya – Tabora ambayo  imebaki kilomita 42.

Viongozi hao  pia walijadili   namna nzuri ya  kuimarisha  uhusiano  katika sekta  mbalimbali  kati ya Tanzania na Korea Kusini, alisema.

“Mazungumzo haya yamejikita katika kuimarisha  maendeleo ya  uchumi,  utamaduni, Tehama (Teknolojia ya Habari na Uhusiano), sayansi, sekta ya utalii na biashara kwa ujumla wake,”alisema Majaliwa.

Alisema wameyapa nafasi kubwa maeneo hayo  na kwamba kwa sasa Watanzania wataanza kuona matunda zaidi kwa uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

“Tumekaribisha  makampuni mengi yaje Tanzania kwa ajili ya uwekezaji, mnajua kuna mradi mkubwa wa reli,   tuna Hospitali ya Mloganzila, zote zinajengwa kwa mkopo wa masharti nafuu  na nchi hii,”alisema Majaliwa.

Alisema  katika mazungumzo hayo na Waziri Mkuu Nak-Yon  pia wamekubaliana kutangaza vivutio  vya utalii vilivyopo nchini kupitia Balozi wa Tanzania   nchini humo, Matunga Masuka.

Alisema  kiongozi huyo  pia amefuraishwa na amani iliyopo  nchini na Tanzania pia  imeipongeza nchi hiyo na nchi jirani ya Korea Kaskazini kwa kukaa pamoja na kuimarisha amani ya eneo hilo.

“Tunaunga mkono juhudi  zao na wameendelea kutuhakikishia kuwa  watajifunza kutoka kwetu   waweze kuimarisha amani baina ya nchi hizo,”alisema Majaliwa.

Katika hafla hiyo pia nchi hizo zilisaini makubaliano ya  kuondoa mahitaji ya viza kwa  watanzania na Wakorea Kusini wanaotumia pasipoti za diplomasia na utumishi.

Makubabaliano hayo yalisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga na Makamu wa Kwanza wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini,  Lim Sang –Nam    kuimarisha uhusiano  na maendeleo ya nchi hizo mbili.

Baada ya kumalizika kwa ghafla hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa na  mgeni wake  walitembelea kituo cha  kuhifadhi kumbukumbu za eletroniki za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)   Kibaha   na Hospitali ya Mnazi Mmoja ambavyo vyote vimejengwa kwa ufadhili wa mashirika ya maendeleo ya nchi hiyo.

Mwisho

 

Uongozi gazeti la Mseto

kurudi mahakamani

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa gazeti la Mseto leo unatarajia kurudi katika Mahakama ya Afrika Mashariki kuiomba kutoa amri ya utekelezaji wa kulifungulia gazeti hilo kama ilivyotolewa katika uamuzi wa kesi hiyo.

Gazeti la Mseto lilifungiwa kwa miaka mitatu kuanzia Agosti 11, 2016 na aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Mwanasheria kutoka Kituo cha Haki za Binadamu na Utawala Bora(LHRC), Fulgence Massawe alisema uamuzi huo ni kutokana na serikali kutoonyesha nia ya kutekeleza uamuzi wa kulifungulia gazeti hilo.

Alisema ni muda mrefu tangu utolewe uamuzi wa kulifungulia gazeti hilo lakini serikali imekaa kimya hivyo wameamua kurudi kuiomba mahakama hiyo kuomba utekelezaji wa uamuzi.

“Kesho Jumatatu (leo), tutarudi tena mahakamani kuiomba iiagize serikali kulifungulia gazeti la Mseto kama hukumu ya mahakama hiyo ilivyoamuru,” alisema Wakili Massawe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles