21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

LUGUMI AVUNJA UKIMYA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, kumsaka na kumfikisha ofisini kwake mmiliki wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, Said Lugumi, mfanyabiashara huyo ameibuka na kuvunja ukimya.

Suala  la kampuni hiyo iliyoingia mkataba na Jeshi la Polisi wa kuweka mashine za utambuzi wa alama za vidole katika vituo 108 vya polisi, wenye thamani ya Sh bilioni 37, ni miongoni mwa maagizo aliyopewa Lugola na Rais Dk. John Magufuli baada ya kuapishwa.

Jana gazeti hili lilimtafuta Lugumi na kuzungumza naye kwa simu ya mkononi ambako alisema yeye si msanii.

Baada ya mfanyabiashara huyo kupokea simu, mwandishi wa MTANZANIA alijitambulisha na akamtaka kulizungumzia agizo la Waziri Lugola lakini alijibu kwa kifupi kuwa yeye si msanii kisha akakata simu.

“Unasemaje (Mwandishi akamweleza nia ya kumpigia simu)… Nasema mimi si msaniii kwa heri,” alisema Lugumi na kukata simu.

Jumamosi iliyopita Lugola alimpa siku 10 Sirro kuhakikisha anamfikisha ofisini kwake mfanyabiashara huyo au ajisalimishe mwenyewe ifikapo Julai 31, saa 2.00 asubuhi.

Lugola alisema si lazima Lugumi asubiri kufuatwa na polisi bali anaweza kufika na kugonga ofisi ya waziri huyo na kujisalimisha.

Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kumpa maagizo IGP Sirro kupeleka taarifa ya kampuni hiyo kufunga vifaa lakini alielezwa   kuwa kazi hiyo ilikuwa haijakamilika.

“Lugumi ni Mtanzania asisubiri polisi, itapendeza akija mwenyewe. Kumbuka waliopita hawakuwa maninja, sasa akija tutajua nini kitatokea, tusubiri,   akifika yatakayojiri tutawaambia Watanzania,” alisema Lugola.

Agosti mwaka jana   Lugumi, alishikiliwa na vyombo vya dola Dar es Salaam  kwa mahojiano.

Kwa mujibu wa vyanzo  ndani ya vyombo vya dola,   mfanyabiashara huyo alishikiliwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles