29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Homa kuelekea Safari ya Beach mabondia watishiana

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

ZIKIWA zimebaki wiki mbili kabla ya pambano la ngumi za kulipwa la lililopewa jina la Safari ya Beach, mabondia watakaopanda ulingoni siku hiyo wameendelea kupigana mkwara kila mmoja akitambia kambi yake.

Pambano hilo linalowakutanisha wakali wa wilaya zote za Dar es Salaam, litafanyika Oktoba 22, 2023 kwenye fukwe za Rongoni, Kigamboni.

Miongoni mwa mabondia hao ni mkongwe Jackson Malinyingi kutoka City Center Gym atakayezichapa Bahari Juma Kijo wa Mabibo, ametamba kuwa yeye ni daraja la kuvusha damu changa hivyo mpinzani wake ajiandae kwa kipigo kizito.

“Mimi niko fiti namuomba Mungu anaifikishe hiyo siku ya tarehe 22, nitamfunza sana na atajua kwamba utu uzima ni dawa na jungu kuu halikosi ukoko. Nimwambie kabisa Chui wa Mabwepande atakuja kunguruma pande za beach,” ametamba Malinyingi.

Naye bondia Bakari Mangosongo, amesema amejiandaa kuipa heshima wilaya yake ya Kigamboni dhidi ya  Yake Ya Kigamboni Kwa Kumtwanga Felix Malume  kwa kumaliza pambano mapema.

Mwingine ni Sebastian Deo wa Chamazi, amemtangazia vita kali  Yohana Daud wa Tegeta Nyuki, huku akiungwa mkono na mashabiki wake ambao wameahidi kutoa sapoti kwa bondia wao  kuhakikisha anamtwanga mpinzani kwa K.O.

Kwa upande Francis Nampumula wa Kijichi, amesema amesikia maneno ya  mpinzani wake Sultani Kiyoko wa  Mbagala Rangi Tatu na kumfanya azidi kupata hasira za kuongeza dozi ya mazoezi ili ampe kipigo cha ufundi.

Zaidi ya mabondia 30 wanarajiwa kupanda ulingoni siku hiyo, huku wanawake wakiwa ni  Zawadi Kutaka dhidi ya Flora Machela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles