23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MANJI KUTOHOJIWA SUALA LA KODI ZA TRA

Na KULWA MZEE- DAR ES SALAAM

MAOMBI ya Jamhuri ya kutaka Mfanyabiashara Yusufali Manji ahojiwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) kuhusiana na masuala ya kodi yamegonga mwamba baada ya mahakama hiyo kukataa kutoa ruhusa hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilikataa maombi hayo ya Jamhuri na kutoa sababu kwamba kesi iliyopo mahakamani inahusu uhujumu uchumi na si masuala ya kodi.

Mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kutaka Manji   akahojiwe na  TRA kuhusiana na masuala ya kodi.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha,   Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alidai awali  waliomba hati ya kumuita mshtakiwa mahakamani lakini kwa sababu za afya hakuweza kufika.

“Leo (jana) yupo mahakamani ni ombi letu achukuliwe na TRA kwa ajili ya mahojiano na ndani ya muda wa kazi atakuwa amerudishwa,”alidai.

Wakili Alex Mgongolwa anayemtetea Manji alidai maombi hayo kwa jana si sahihi kwa kuwa walikwisha kufanya mawasiliano ya maandishi na TRA.

Mgongolwa alidai Manji anao mawakili wengine wanaoshughulika na masuala ya kodi hivyo anahitaji kuwasiliana nao ili mahojiano hayo yawe na manufaa.

Alihoji kuhusu mahojiano hayo kwamba anatakiwa Manji ama makampuni yake.

Kishenyi alidai anayehitajiwa katika mahojiana hayo ni Manji na siyo makampuni yake na kwamba akifika huko akaona kuna hana ya kuwa na wataalamu wake atasema.

Hakimu Mkeha baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema hawezi kukubaliana na ombi hilo kwa kumruhusu Manji kwenda TRA kwa sababu kesi iliyopo mbele yake ni ya uhujumu uchumi na haihusiani na masuala ya kodi.

Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hadi Agosti 18, 2017 kwa ajili ya kutajwa na aliwaambia kwa kuwa mshtakiwa yuko katika maeneo ya mahakama watumie utaratibu  wanaoona unafaa kukamilisha wanachohitaji.

Katika kesi hiyo, Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwamo ya kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 na mihuri.

Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni  Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere

Kesi hivyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye amefiwa na mama yake mzazi hivyo kesi ikatajwa kwa Hakimu Mkeha.

Manji na wenzake wanadaiwa kuwa Juni 30,2017 katika eneo la Chang’ombe ‘A’wilaya ya Temeke Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa na polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),  zenye thamani ya Sh milioni 192.5 na kwamba mali hiyo ilipatikana kinyume cha sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles