Harmonize, Ali Kiba kunogesha Wasafi Festival

0
1261

BRIGHITER MASAKI

TAMASHA la ‘Wasafi Festival’ linatarajiwa kufanyika Novemba 9, mwaka huu katika viwanja vya Sayansi jijini Dar es Salaam huku msanii Harmonize, Ali Kiba wakitarajiwa kupagawisha mashabiki.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo Mkurugenzi wa Wasafi Media, Diamond Platnum, amesema tamasha hilo litafanyika kwa mara ya kwa jijini Dar es Salaam, hivyo mashabiki watarajie burudani ya kutoka kutoka kwa wasanii wakubwa nchini.

“Tamasha linafanyika kwa mara ya kwanza Novemba 9 katika viwanja vya Sayansi, kutakuwa na burudani tofauti kutoka kwa wasanii wa Tip Top, Wanaume Family, muziki wa Kisengeli pamoja Tarabu.

“Babu Tale alimpigia simu Ali Kiba kuwa anatakiwa kufanya shoo kwenye Wasafi Festival ili kuonyesha umoja uliopo kwa wasanii, mwingine ni Harmonise naye ataimba kwa kuwa hapa ni kama nyumbani kwake,” alisema Diamond.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here