27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yazindua kampeni mpya kwa wateja wao inayoitwa “VUNA POINTI”

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu ya Halotel leo Februari 23, 2024 imezindua kampeni nyingine mpya kwa wateja wake inayofahamika kama Vuna Pointi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu wa Sekta ya Biashara wa Halotel, Abdallah Salum amesema Vuna pointi ni kampeni ambayo Halotel inaonyesha kujali na kuthamini wateja wake wajisikie wao ni wathamani hasa katika kupata huduma nzuri za mawasiliano. 

“Vuna pointi ni kampeni ya wateja wanaoonyesha uaminifu wa kutumia mtandao wa Halotel kwa kupata bonasi ya pointi kila akionge muda wa maongezi kupitia vocha ya kukwangua au kwa Halopesa pia kwa kufanya miamala ya pesa na pia kwa kununua vifurushi kwa Halopesa,” amesema.

Amefafanua zaidi kuwa Pointi hizo za bonasi zinaweza kuvunwa na kuwa dakika, SMS au MB.

“Mteja anaweza kuvuna pointi kwa kupitia MyHalo App au kwa kupiga *148*66# kisha chagua VUNA POINT. Pointi zilizovunwa zinaweza kubadilishwa na kuwa SMS, dakika, MB au namba ya Bahati itakayotumika kushiriki michezo ya Bahati nasibu ya Halotel,” amesema Salum na kuongeza kuwa:

“Halotel itaendelea kutoa huduma bora kwa gharama nafuu huku tukiendelea kuwa karibu na wateja wake kila siku, kwa kubuni na kuzindua michezo mbali mbali  kama sehemu ya kendeleza burudani na kufurahisha wateja wetu kwa kuchagua mtandao wetu wa Halotel katika huduma za mawasiliano nchini,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles