29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Halopesa yazindua Promosheni ya OKOTA na HALOPESA

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel katika kuelekea Msimu wa Sikukuu, imezindua Promosheni ya “Okota na Halopesa ambapo watumiaji wote wa mtandao huo kote nchini watanufaika.

Akizungumza na Waaandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2023 Afisa Masoko wa Halotel, Roxana Kadio, amesema ni furaha kwao kutambulisha bidhaa hiyo kwa wateja wao kwani inatoa fursa kwao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo fedha taslimu hadi Sh milioni moja.

“Mteja wetu kila unapotumia Halopesa Lipa hapa kupitia 15088# au kufanya miamala mbalimbali kwa kutuma pesa kwenda Halotel au mitandao mingine na kwenda benki ambapo zaidi ya wateja milioni 3.5 wataendelea kufurahia huduma zenye ubora muda wowote kupitia promosheni hii,” amesema Roxana.

Amesema kampeni hii imelenga kuwazawadia wateja wa Halotel katika Msimu wa sikukuu kila anapofanya miamala ya Lipa hapa kupitia USSD na miamala mingine itakayomuwezesha kuingia katika droo ya kila siku, wiki na mwezi.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Bishara Halopesa, Joseph Jackson, amesema kuwa kampeni ya Okota na Halopesa ni kwa ajili ya wateja wa Halopesa ambayo itakuwepo kwa miezi mitatu ambapo jumla ya wateja 300 watakuwa washindi huku kila mteja wa Halopesa akiombwa kushiriki katika droo hiyo kwa kufanya miamala mingi.

“Halopesa inafurahia kuzindua Promosheni hii na itaendelea kufikiria njia nyingine zaidi za kufanya ulimwengu wa huduma za kifedha kupitia simu kuwa bora zaidi kwa ajili ya wateja wetu,” aalisema Jackson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles