23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

HAKIMU KESI YA ‘SCOPION’ MGONJWA

FARAJA MASINDE Na CAROLINE CHALE (TUDARCO) -DAR ES SALAAM

KESI ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi, ikiwamo kumtoboa macho Said Mrisho, inayomkabili Salum Njwete (34) maarufu ‘Scorpion’, imeahirishwa hadi Septemba 11, mwaka huu baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule kuwa mgonjwa.

Kesi hiyo ambayo ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi, Adelf Sachore kwa kuongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga.

“Shauri hili linakuja kwa ajili ya utetezi upande wa waleta maombi kwenye kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, hata hivyo hakimu anayesikiliza shauri hili, (Flora Haule) ni mgonjwa, hivyo mimi pamoja na Wakili wa Mshtakiwa, Juma Nassoro tulikuwa tunaomba kwa pamoja kama itakupendeza tuendelee Septemba 11, mwaka huu,” alidai Katuga.

Hakimu Sachore alikubali maombi hayo ya upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 11, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja tena.

Upande huo wa utetezi ulifungua kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi baada ya kile ilichodai kuwa ‘Scorpion’ alilazimishwa kutoa maelezo kwa nguvu katika kituo cha polisi Buguruni, jambo ambalo lilipingwa na shahidi wa tisa, DC Bryson ambaye alidai kuwa alifanya mahojiano na mtuhumiwa kwa amani na kwa uhuru.

Hoja nyingine ambayo iliwasilishwa na upande huo wa utetezi ilikuwa ni kupinga mahakama kupokea maelezo yaliyowasilishwa na shahidi aliyemfanyia mahojiano Scorpion kwa madai kuwa yalikiuka kanuni na hivyo kuzuia mahakama hiyo kuyapokea kama kielelezo.

Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa Septemba 6, mwaka huu saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, mshtakiwa aliiba cheni ya silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000 na black bendi ya mkononi na fedha taslimu Sh 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles