25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

DK. TULIA ATOA MSAADA WA TELEVISHENI JKCI

NA ABDALLAH NG’ANZI (Tudarco)

NAIBU Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amehimiza taasisi za umma na mashirika binafsi kuendelea kutoa misaada katika sekta ya afya ili kupunguza changamoto zinazoikabili.

Dk. Tulia ameyasema hayo jana baada ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na kukabidhi msaada wa televisheni, ving’amuzi vinne na katoni mbili za maziwa.

“Jukumu la kuijali afya ni la kila mmoja wetu, ni vizuri tukajitoa katika hili na kwa upande wangu nimeanza na hivi, nawaomba wananchi na mashirika mbalimbali wajitokeze kwa wingi kutoa misaada ili kuweka mazingira mazuri kwa wagonjwa kujisikia huru,” alisema Dk. Tulia.

Mwakilishi wa Kampuni ya TSN, Jahu Mohammedi, alisema msaada huo utawasaidia wagonjwa kufuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammedi Janabi, alimshukuru Naibu Spika kwa msaada huo na kuomba wahisani waendelee na moyo huo kwani changamoto zinazoikabili taasisi hiyo bado ni nyingi.

Wakati huo huo, daktari bingwa wa tiba ya moyo, Dk. Peter Kisenge amewashukuru wataalamu wanne wa upasuaji kutoka China waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini.

Dk. Kisenge ambaye alikuwa mwenyeji wa wataalamu hao, alisema madaktari hao wameishi nchini na kutoa huduma za upasuaji katika taasisi hiyo kwa muda wa miaka miwili na kufanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 300.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles