30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAUZO DSE YAPOROMOKA

JOHANES RESPICHIUS Na SHABANI CHUWAKA (TUDARCo) -DAR ES SALAAM

THAMANI ya mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imepungua kutoka Sh bilioni 7.5 wiki iliyopita hadi Sh bilioni 6 wiki hii baada ya hisa zimeuzwa na kununuliwa kushuka kutoka hisa milioni 31 hadi kufikia laki 8.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa DSE, Mary Kinabo, alisema licha ya mauzo kushuka ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko uliongezeka.

“Ukuba wa mtaji wa kampuni zilizoorozesha sokoni umeongezeka  kwa Sh bilioni 357 hadi kufikia Sh trilioni 20.9 kutoka Sh trilioni 20.6 wiki iliyopita ikichangiwa na kupanda kwa bei ya hisa za Acacia  kwa asilimia 12, NMG asilimia 10, KA asilimia 9, DSE asilimia 3 na TBL kwa asilimia 2.

“Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Sh bilioni 89 kutoka Sh trilioni 9.7 hadi Sh trilioni 9.9 ikitokana na kupanda kwa bei ya hisa za DSE kwa asilimia 3 na TBL asilimia 2,” alisema Mary.

Kuhusu viashiria vya soko, Mary alisema kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa sokoni kilipanda kwa pointi 37 kutoka pointi 2,142 hadi 2,179 baada ya kushuka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali.

Alisema kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI nacho kilipanda kwa pointi 34 kutoka 3,728 hadi 3,763 hivyo hivyo kwa sekta ya viwanda ambayo ilipanda pointi 78 hadi kufikia pointi 4,870 kutoka 4,792 baada ya hisa za TBL kupanda bei asilimia 2 kutoka Sh 13000 hadi Sh 13,363.

“Kiashiria huduma za kibenki na kifedha kilipanda kwa pointi 1 kutoka pointi 2,605 hadi pointi 2,606 huku sekta ya huduma za kibiashara ikibaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,475,” alisema Mary.

Alisema mauzo ya hati fungani yaliongezeka kutoka Sh milioni 192 wiki iliyopita hadi Sh bilioni 5.7 yakitokana na hatifungani sita za serikali zenye thamani ya Sh bilioni 6.5 kwa gharama ya Sh bilioni 5.7.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles