25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Gumzo Trump kuteuliwa kuwania tuzo amani ya Nobel

 WASHINGTON, MAREKANI

MSHANGAO na mijadala imeibuka baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuteuliwa kwa mara ya pili kuwania tuzo ya amani ya Nobel.

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Norway amelipendekeza jina la Trump kuelekea tuzo hizo za mwaka 2021, akieleza kazi ya rais huyo katika mpango wa hivi karibuni wa kuleta amani kati ya Israel na Umoja wa falme za kiarabu.

Christian Tybring-Gjedde alikiambia chombo cha habari cha Fox News siku ya Jumatano ‘’Ninafikiri amefanya zaidi katika kutafuta amani kati ya mataifa kuliko ilivyo kwa wateuliwa wengine wa tuzo hii.’’

Ameongeza kuwa yeye hakuwa mtu anayemuunga mkono sana Trump,aliongeza. ‘’Kamati inapaswa kuangalia ukweli na kuamua kwa kutazama ukweli wa mambo, na si kwa namna anavyoonesha tabia zake mara kadhaa.’’

“Hakika kuteuliwa si sawa na kushinda- hatutamjua mshindi kwa miezi mingine 13 ijayo” alisema.

Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na kuteuliwa kwake huko.

Wengi wameonekana kuonyesha mshangao, wengine wakihoji kikubwa alichokifanya ukilinganisha na watangulizi wake.

 Maprofesa wa vyuo vikuu, Wakurugenzi wa Taasisi za sera za mambo ya nje, washiriki waliopita wa tuzo ya Nobel wajumbe wa kamati ya tuzo ya nobel nchini Norway pia ni miongoni mwa wale waliofuzu kuwasilisha uteuzi wao kwa ajili ya tuzo hiyo.Teuzi hizo hazihitaji mualiko

Kwa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2020- mshindi ambaye bado hajatangazwa- kulikuwa na watu 318 wanaowania.

Kamati ya Nobel ya Norway haitoi maoni hadharani kuhusu wanaowania, ambao hufanyika kuwa siri.

Trump anachaguliwa kuwania tuzo hizo kwa mara pili na Tybring-Gjedde mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2018.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia alikua miongoni mwa wabunge wawili waliomchagua Trump kwa ajili ya tuzo hiyo hiyo, kutokana na jitihada za kupatanisha Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Trump hakushinda tuzo hiyo mwaka huo, lakini Tybring-Gjedde, wa chama wa Conservative Progress Party, anasisitiza kuwa Rais Trump awamu hii ametimiza vigezo.

Mwezi uliopita, Israel na UAE walifikia makubaliano ya kusawazisha mahusiano yao, huku Israel ikikubali kuahirisha mipango yake ya kupokonya sehemu ya eneo linalokaliwa la ukingo wa magharibi- hatua iliyotangazwa na Trump.

Trump ni mmoja kati ya marais wa Marekani kupata uteuzi huo, wakiwemo Rais William Howard Taft, Rais Herbert Hoover na Rais Franklin Roosevelt.

Uteuzi wa Obama kwa ajili ya tuzo ya amani ya Nobel ilisababisha ukosoaji mkubwa

Ikiwa atapata tuzo hiyo, Trump atakuwa rais wa tano wa Marekani kushinda, akiwafuatia Theodore Roosevelt mwaka 1906. Woodrow Wilson mwaka 1920, Jimmy Carter mwaka 2002 na Barack Obama mwaka 2009.

 Ushindi wa Obama- ambao uliotokea miezi kadhaa tu akiwa katika wadhifa huo mkubwa – ulikutana na ukosoaji nchini Marekani, huku baadhi wakisema hakuna alichofanya cha kustahili kupata tuzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles