26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama Ubelgiji yatoa amri jino la Lumumba lirudishwe

 BRUSSELS, UBELGIJI

MAHAKAMA mjini Ubelgiji imeamuru kwamba jino lililochukuliwa kutoka kwenye maiti ya shujaa wa Uhuru wa taifa la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Patrice Lumumba lirejeshwe kwa familia yao.

Lumumba aliyekuwa waziri mkuu wa Congo baada ya kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960, aliuawa 1961 baada ya kutekwa na wapiganaji waliotaka kujitenga.

Serikali ya Ubelgiji ilihusika katika kifo chake na mwaka 2002 iliomba msamaha rasmi.

Vitengo vya ujasusi vya Uingereza na Marekani pia vinadaiwa kuhusika.

Jino la Lumumbua linadaiwa kuchukuliwa na ofisa wa polisi wa Ubelgiji aliyekuwa anasaidia kuuzika mwili wake , chombo cha habari cha AFP kimeripoti.

Baadaye jino hilo lilichukuliwa na mamlaka ya Ubelgiji , AFP kinaongezea.

Mahakama hiyo ya Ubelgiji ilisema kwamba jino hilo sasa linafaa kupewa mtoto wa kike wa Lumumba, Juliana Lumumba , ambaye aliandika barua kwa mfalme huyo wa Ubelgiji akiomba lirudishwe, mtandao wa Brussels Times uliripoti.

Kulingana na mtandao huo uamuzi huo wa mahakama siku ya Alhamisi unatokana na uamuzi mwingine wa ofisi ya kiongozi wa mashtaka wa kijimbo kwamba mabaki ya Lumumba yanaweza kurudishwa kwa familia yake.

Hatua ya Ubelgiji kurudisha jino la Patrice Lumumba kwa familia yake kumepokelewa vyema na familia hiyo.

Mpwa wake, Jean Lumumba anasema kwamba familia yake haikumzika kwasababu mwili wake ulitiwa ndani ya tindi kali uangamie.

“Lumumba ni shujaa ambaye hakuzikwa , hatua ya mahakama ya Ubelgiji ni njema kujua ukweli,” alisema Jean Jacques .

Alisema kwamba wanaume wawili Joseph Okito na Maurice Mpolo ambao waliuawa pamoja na Lumumba pia ni mashujaa wa Congo na kwamba ukweli kuhusu mauaji yake unafaa kufichuliwa.

Mwaka 2000, Gerard Soete, kamishna wa polisi wa zamani nchini Congo akiwa na miaka 80 wakati huo aliambia AFP kwamba alimkatakata Lumumba na wenzake na kuweka miili yao ndani lakini akachukua jino lake.

Soete alifariki miaka michache baadaye baada ya kutoa ushahidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles