27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Gladness agawa vifaa vya kujikinga na corona

JEREMIA ERNEST

Muigizaji wa vichekesho nchini, Gladness Kifaluka ‘Pili’ amegawa vifaa na vitakasa mikono kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu unayosababishwa na virusi vya corona.

Msanii huyo anayefanya vizuri kwa sasa katika tasnia kupitia kipindi chake cha Kitim tim amesema ameona ni vema kugawana na jamii kidogo alichonacho katika kpindi cha janga hili kubwa.

Gladness ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Machi 30, alipokuwa akiazungumza na waandishi wa habari katika ofisi za serekali ya mtaa wa Makumbusho.

“Tunashukuru nchini kwetu bado tuna nafasi ya kufanyia kazi sio kama wenzetu leo nimeamua kuja kugawa vifaa vya kujikinga na ugonjwa huu kwa watu ambao bado hawajavipata,” amesema Gladness.

Aidha ameishukuru serikali kwa hatua mbazo imechukua ili kuinusuru jamii na janga hilo pia ametoa rai kwa makampuni na watu binafsi wenye uwezo kusaidia watu ambao hawana kwa kipindi hiki cha mpito.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles