Gigy Money aililia ndoa

0
1308

Na GLORY MLAY

MSANII wa bongo fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka na kusema kwa sasa anatamani kuolewa ili kuona utamu wake. 

Akizungumza na MTANZANIA jana, Gigy alisema hakuna mwanamke yeyote anayetaka kuzeeka bila kuingia kwenye ndoa.

“Sidhani kama kuna mwanamke ambaye hajaingia kwenye ndoa na hatamani kuingia, kwa upande wangu kwa vile sijaingia, kwa kweli natamani sana kuwa na ndoa ili niwe na mume wangu peke yangu,” alisema 

Alisema yupo tayari kuolewa na akitokea mwanaume ambaye amempenda basi itakuwa jambo la heri kwake yeye na familia yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here