23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

GGML yazindua Kampeni ya GGM Kili Challenge 2022

*Kukusanya zaidi ya Sh milioni 500

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imezindua harambee ya uchangia kampeni ya GGM Kili Challenge Mwaka 2022 kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.

Katika kampeni ya mwaka huu GGM inakusudia kukusanya kati ya Sh milion 500 hadi bilion moja ikiwa na lengo la kuisaidia Serikali katika jitihada zake kufikia malengo ya sufuri tatu.

Meneja Mwandamizi kutoka GGM anayehusika na Ubia, Manace Ndoroma amasema mwaka huu wameendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi hivyo GGM kwa kushirikiana na TACAIDS wanatarajia kuanza kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Julai 15 hadi 21, mwaka huu.

Amesema takwimu za Kitaifa za watu wanaoishi na VVU hujuimuisha hata wale wanaoishi mkoani Geita na kwamba wanafanya jitihada za pamoja kutokomeza maambukizi mapya nchi nzima.

Amesema GGM Kili challenge imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 hadi kufikia kuwa mfumo wa kimataifa unaoshirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli zaidi ya 700 kutoka mabara sita na zaidi ya nchi 20.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ametoa wito kwa wananchi na vijana kuendelea kuchukua tahadhari dhidi VVU na UKIMWI ambapo amesema licha ya kupungua kwa maambukizi mpya jitihada zaidi inahitajika katika kukabiliana na janga hilo.

Kagaigai amesema kuwa katika tukio hilo huduma mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu na upimaji wa VVU, elimu ya chanjo ya Uviko-19 pamoja na uchangiaji damu.

Amesema fedha zitakazopatikana zaidi ya nusu zitaenda kwenye NGO’s ambazo mara nyingi zinakuwa zinaendeshwa na Watanzania kusaidia kwenye jamii katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amesema takwimu zinaonyesha kuwapo kwa ongezeko la maambukizi mapya ya VVU hususani kwa makundi maalum yaliyo katika hatari kubwa hadi kufikia mwaka 2020 idadi ya Watanzania wanaioshi na VVU walikuwa watu milioni 1.7 huku maambukizi mapya kwa mwaka 2020 yalikuwa ni watu 68,000.

Dk. Maboko amesema makundi yaliyo katika hatari ya kupata maambukizi ya VVu ni vijana, wanaotumia madawa ya kulevya, wanaofanya biashara ya ngono, madereva wa masafa marefu, wafanyakazi wa kwenye mashamba makubwa na jamii za wavuvi na wafanyakazi wa migodini.

Amesema Vifo vinavyotokana na UKIMWI ndani ya miaka 10 iliyopita vimepungua kwa asilimia 50 na kwamba mwelekeo ni mzuri ambapo maambikizi yanapungua, vifo navyo vinapungua kwasababu watu wanapima, wanaanza dawa na wengine wanaendelea kunywa dawa.

“Kupitia hizi shughuli za kupanda mlima kwa miaka 20 fedha zilizopatikana katika kipindi hicho ni takribani Sh bilioni 12 na kila mwaka kipindi cha nyuma tulikuwa tukipata Sh milioni 500 hadi 700 na mwaka huu tunaamini hatutakosa Sh milioni 500 hadi Sh bilioni 1 na ndio lengo letu hili,”amesema Dk. Maboko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles