31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Vodacom yaahidi kuendelea kuwawezesha Watanzania, Meya aipongeza

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwanyanyua Watanzania kiuchumi hasa wa kidigital.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kidigital wa kampuni hiyo, Nguvu Kamando akwenye maonyesho ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema Vodacom imekuwa ikibuni mbinu mbalimbaki za kumwezesha mkulima au mfanyabiashara wa Tanzania kuweza kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa njia rahisi.

“Sisi Vodacom ni wadau wa maaendeleo nchini sio tu kuboresha huduma za kimaendeleo pia tunamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumfikia Mtanzania mmoja mmoja ili kuweza kutoa tija katika biashara zake,” amesema Kamando.

Amesema kwasasa wana miradi mbalimbali ikiwamo ule wa kumsaidia mwanamke mwemye kipato cha chini kuweza kupata mkopo kidigitali bila kusahau wakulima na wafanyabiashara.

Upande wake Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto ameipongeza kampuni hiyo kwa kusogeza huduma za kijamii kwa Watanzania.

“Nimefarijika kuona Vodacom haikujiachia tu na mchezo wa kubahatisha lakini nimeona shuhuli za kilimo, uchumi, biashara na fursa nyingine jukumu letu kama Watanzania ni kuweza kupata huduma zenye ufanisi,” amesema Kumbilamoto.

Kumbilamoto pia alimkabidhi gari mshindi wa TUSUA MAPENE kutoka jijini Dar es Salaam nakwamba amefarijika kuona gari hilo likibaki kwenye jiji lake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles