29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC kujenga vituo vitano vya gesi asilia nchini

Na Hadia khamis, Mtanzania Digital

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linatarajia kujenga vituo vitano vya gesi asilia hadi kufikia Desemba, mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya 16 Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio amesema vituo hivyo vitasaidia kupunguza malalamiko ya kuwa na vituo vichache vya gesi asilia.

Amesema mpaka sasa TPDC imegundua kiasi cha gesi futi za ujazo Trillion 57.54.

“Kiasi kikubwa cha gesi kipo baharini, tunatarajia kukivuna, kwasasa tunaendelea na mtambo wa LNG ambao utachakata gesi hiyo,” amesema Dk. Mataragio.

Amefafanua zaidi kuwa baada ya kuchakatwa gesi itapoozwa hadi kufikia juzi joto 160 ambapo itasafirishwa kwenda kwenye masoko ya nje na kwamba kiasi kitakachobaki kitatumika kwa ajili ya soko la ndani.

“Mteja atakuwa anaenda kwenye vituo vyetu ili kuweza kuweka gesi anayoihitaji, matumizi makubwa ya gesi asilia ni kuzalisha umeme ambapo gesi inachangia asilimia 62 kwenye gridi ya taifa.

“Na asilimia 20 ya gesi imekuwa ikitumika kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani ambapo magari yanatumia gesi ya CNG,” amesema Dk. Mataragio.

Aidha, aliwataka Watanzania kutarajia matunda yatakayopatikana kutokana na gesi asilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles