24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

GGM wachangisha zaidi ya bilioni mbili mapambano dhidi ya Ukimwi

Upendo Mosha – Moshi

Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali wamefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni mbili Katika kampeni yake ya mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Akizungumza wakati akiwapokea wapandaji wa Mlima Kilimanjaro 32 na waendeshaji wa baiskeli 32 ambao walizunguka Mlima huo  kwa lengo la kuhamasisha uchangishaji wa fedha hizo jana Juni 21, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira, alisema kuwa kupitia mfuko maalumu ya kusaidia  kampeni  ya mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwili kwa mwaka huu wamefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni mbili fedha ambazo zinatoka na wafadhili pamoja na wadau wengine.

“Katika kipindi Cha miaka 17 tangu GGM wameanzisha kampeni hii wamefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 13 mbali na fedha hizo kwa mwaka huu kupitia kampeni hii wamechangisha zaidi ya Bilioni mbili ambazo zinatokana na wafadhili na wadau wengine” alisema.

Naye Makamu wa Rais wa (GGM) Simon Shao, alisema kupitia kampeni hiyo zaidi ya taasisi 50 zinazojihusisha na masuala ya ukimwi zimenufaika kupitia fedha hizo ikiwemo kituo Cha kulelea watoto yatima cha Moto wa Huruma.

“Tumekuwa tukichabgisha fedha hizi za mapambo dhidi ya virusi vya Ukimwi kwa miaka 17 fedha zinazopatika tunazitumia kusaidia mapambano haya, toka tumeanza zaidi ya watu 800 wamepanda Mlima Kilimanjaro na leo zaidi ya asilimia 99 wamefika kileleni” alisema.

Mbali na hilo alisena GGM itaendelea kushirikiana na serikali Katika masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo mapambano dhidi ya Ukimwi na kwamba ni vyema taasisi nyingine zikashiriki Katika kampeni hiyo na kuacha kuitegemea serikali pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles