21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tatizo la taulo za kike latesa wanafunzi Maswa

 Samwel Mwanga-Maswa

Ukosefu wa taulo za kike katika shule za msingi wilaya ya Maswa mkoani
Simiyu limeendelea kuwa tatizo kwa wanafunzi wa kike hali inayopelekea kushindwa kuhudhuria masomo wakati wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wanafunzi wa kike walioko katika kambi ya
kitaaluma katika shule ya msingi Binza iliyopo wilayani hapa kwa wanafunzi wa darasa la saba walipokuwa wakizungumza na MTANZANIA
ilipowatembelea katika kambi hiyo kuona changamoto zinazowakabili.

Walisema kuwa sasa umefika wakati kwa serikali kuweka utaratibu
madhubuti  utakaowawezesha kupata hitaji hilo maalum lenye  msingi wa
kulinda afya zao.


“Ni lazima sasa tufunguke juu ya suala hili la taulo za kike kuwepo
katika shule zetu za msingi wanafunzi wa kike hatuna haja ya kuficha
ni lazima tuwe wazi kwani tunaathirika sana kwa kukosa
vipindi tunapokuwa katika kipindi cha hedhi hivyo ni vizuri serikali
ikaona umuhimu wa kuweka bajeti ya kununua taulo hizo katika shule
zetu iwe ni sehemu ya sisi kupata elimu bila malipo,” amesema mmoja wa wanafunzi Fatuma Ally.

Aidha wanafunzi hao wamesema kuwa licha ya utaratibu mzuri uliowekwa na serikali ya mkoa wa Simiyu ya kuwaweka katika makambi hayo lakini zipo sababu nyingi zinazochangia kudumaa kwa ustawi wa elimu ya mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na uhaba wa taulo za usafi wakati wa hedhi kwani wanakuwa na hofu ya kupoteza thamani ya utu wao hasa shuleni.

 “Hali hii hutufanya baadhi yetu kutohudhuria darasani na matokeo yake wengine wasio wavumilivu hufikia uamuzi wa kuacha shule
na taifa litakosa wasomi mahiri kwa siku zijazo,” amesema Magreth
Joseph.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles