27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

GF Trucks & Equipment Ltd yaipa Nguvu Timu ya Jeshi la Polisi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya magari ya GF Trucks & Equipment imeikabidhi vifaa vya michezo timu ya Jeshi la Polisi Zanzibar lengo likiwa na kuimarisha michezo na kukuza ushirikiano.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Zanzibar Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Salman Karmali ameilipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwa sehemu kubwa ya wadau wa michezo visiwani humo.

Amesema kampuni ya GF Trucks & Equipment LTD imekuwa sehemu kubwa ya michezo Tanzania Bara na kwamba kwa sasa imeamua kugeukia upande wa Zanzibar.

“Ndani ya miaka 15 tunayosherekea leo, GF Truck tumeweza kushirikiana na timu kadhaa Mbao FC, DTB na sasa Singida Big Stars inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC, hii inatupa matumaini kuendelea kutoa ushirikiano kwenye sekta ya michezo.

“Leo hii tunakabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Polisi ambazo ni jezi na soksi ikiwa ni sehemu ya kusapoti sekta ya michezo kwa huku Zanzibar, nasi tutaendelea kuangalia kwa namna gani tunaweza kuipa nguvu michezo kwa huku kisiwani. Hii ni kutokana na miaka ya 15 ya kibiashara ya GF Trucks kuwepo kwenye soko,” amesema Karmali.

Aidha, amesema kupitia kampeni ya Royal Tour na Uchumi wa Bluu sisi kama wadau wa maendeleo wanampongeza sana Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi na viongozi wengine visiwani humo katika kuhamasisha maendeleo.

“Sisi ni wadau wakubwa wa sekta ya maendeleo ya ujenzi, miundombinu na ujuzi tuna amini kufungua milango ya kibiashara kwa Zanzibar kupitia kampuni za ujenzi, wakandarasi na wachimbaji kupitia chapa zetu (brand) mbili za FAW Magari makubwa na XCMG Machine inayohusisha Excavator.

“Pia tunatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri na hongereni kushiriki sekta ya michezo. Nimalizie kwa kusema kwa pamoja tukashiriki kwenye Sensa ambayo itafanyika Agosti 23 mwaka huu nchini kote ili iweze kuisaidia Serikali kupanga maendeleo,” amesema Karmali.

Upande wake Kamishana, CP Hamad Khamis Hamad wa Jeshi la Polisi Zanzibar akipokea vifaa hivyoameishukuru kampuni hiyo ya GF Trucks kwa udhamini huo na kuahidi kuendeleza uhusiano baina ya Jeshi la Polisi na GF Trucks.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles